HabariNews

Mtu mmoja afariki huko Nairobi baada ya kuangukiwa na ukuta….

Mtu mmoja amefariki katika mtaa wa makadara jijini Nairobi baada ya ukuta wa nyumba iliokuwa ikibomolewa kuporomoka na kumuangukia.

Marehemu Hananatan Ouma alikumbana na mauti yake  wakati familia  zaidi ya 8 zilipokuwa zikifurushwa kwenye kipande cha ardhi chenye utata.

Kulingana na wenyeji ardhi hiyo ni mali ya kaunti ya Nairobi lakini imenyakuliwa na mwekezaji wa kibinafsi.

BY NEWS DESK