HabariKimataifaNews

Umoja wa Mataifa una wasi wasi juu ya kutorejea kwa malori ya misaada yanayoenda Tigray.

Umoja wa Mataifa umeelezea hofu kwamba mamia ya malori yaliyobeba misaada kuelekea katika jimbo la kaskzini mwa Ethiopia la Tigray hayarudi.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini humo wanasema hakuna lorihata moja kati ya malori 149 yaliyokuwa katika msafara ulioelekea katika mji mkuu wa Tigyar Bekele wiki iliyopita ambalo limerudi.

Wameongeza kuwa tangu tarehe 12 Julai, ni malori 38 pekee kati ya malori 466 ambayo yameingia Tigray na kurudi:

Serikali ya Ethiopia inasema inashuku waasi wa Tigray wamekuwa “wakiyachukua malori hayo kwa ajili ya shuguli zao ”, kulingana na ukurasa wa twitter unaohusiana na serikali.

BY NEWS DESK