HabariKimataifaNews

RAIS WA ZAMANI WA ALGERIA ABDULAZIZ BOTEFLIKA AFARIKI DUNIA….

 

Rais wa zamani Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki dunia

Abdelaziz Bouteflika, alieitawala Algeria kwa miongo miwili kabla ya kujiuzulu 2019 kufuatia maandamano makubwa ya kupinga muhula wa tano, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84, televisheni ya umma imetangaza.

Mtawala huyo wa zamani aliondoka madarakani Aprili 2019 chini ya shinikizo kutoka jeshini, kufuatia wiki kadhaa za maandamano ya kupinga azma yake ya kuwania muhula wa tano madarakani.

Baada ya kujiuzulu, hakuonekana tena hadharani na alisalia kwenye makaazi yake mashariki mwa mji mkuu wa Algiers.

Bouteflika alichaguliwa rais wa Algeria mwaka 1999 wakati koloni hilo la zamani la Ufaransa likitoka kwenye vita vya muongo mmoja vilivyosababisha vifo vya watu karibu 200,000.

BY NEWS DESK