AfyaHabariMombasaNews

Madkatari kaunti ya Mombasa kurudi kazini hapo kesho…………

Ni rasmi sasa kwamba madaktari katika kaunti ya Mombasa watarudini kazini hapo kesho

Kulingana na katibu wa muungano wa madaktari KMPDU ukanda wa pwani Shaban Nassir, hatua hio imeafikiwa baada ya kikao na kamati ya kitaifa ya KMPDU pamoja na serikali ya kaunti ya Mombasa, kuwa watalipwa baadhi ya marupurupu pamoja na mshahara wa mwezi agosti.

Aidha Nassir ameongeza kwamba iwapo serikali ya kaunti ya Mombasa haitaafikia kukamilisha ahadi yake, basi madaktari hao hawatakuwa na budi ila kuendeleza mgomo wao.

Nassir vilevile amesema kwamba kamati ya kitaifa imeahidi kushtaki wale wote waliotia saini makubaliano na madaktari hao ya mwaka 2015 pamoja na bima ya NHIF.

Madaktari hao walikuwa wamesusia kazi kutokana na kudai mishahara yao ya miezi miwili, bima ya NHIF pamoja na marupurupu mengine.

BY NICK WAITA