HabariMombasaNews

Ni afueni kwa familia ya Abdulhakim Saggar…

Hatimaye Abdulhakim Saggar ameachiliwa huru.

Wakizungumza na wanahabari, baadhi ya viongozi kaunti ya Mombasa, Jamaa na marafiki wa Saggar, wamesema kuwa Saggar amerudi nyumbani akiwa salama baada ya kuachiliwa huru katika barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi usiku wa kuamkia leo.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir pamoja na Seneta wa Mombasa Mohammed Faki, wamekashfu kitendo hicho cha Saggar kuachwa njiani usiku sawia na utekaji nyara na kuitaka serikali kuwajibika katika kuwalinda wananchi.

Hata hivyo wametaka haki ipatikane kwa Saggar .

Ikumbukwe kuwa Saggar alitekwa nyara tarehe 18 mwezi agosti katika mtaa wa Old town kaunti ya Mombasa kwa madai ya kujihusisha na ugaidi.

BY NATASHA TALU