HabariNews

Misokoto 149 ya bangi yanaswa katika kijiji cha Burani kaunti ya Kwale…

Maafisa wa polisi katika eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale wamenasa jumla ya

Kamanda wa polisi kaunti hiyo Ambrose Steve Oloo amesema kuwa bangi hiyo ya thamani ya zaidi ya shilingi elfu 20 ilinaswa baada ya polisi kufanya msako katika nyumba moja eneo hilo.

Aidha, Oloo amedokeza kwamba maafisa hao walimkamata mshukiwa mmoja anayetarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho baada ya kupatikana na bangi hiyo.

Kamanda huyo amesema kuwa sasa bangi hiyo itapelekwa katika maabara ya serikali ili kufanyiwa uchunguzi.

Hata hivyo, Oloo amewataka wananchi kudumisha uhusiano mwema na polisi ili kuwakabili walanguzi wa dawa za kulevya.

BY REPORTER