HabariMombasaNews

Maafisa watano wa polisi wanaokabiliwa na kesi ya mauaji wamekana mashtaka dhidi yao…

Maafisa watano wa polisi wanaokabiliwa na kesi ya mauaji eneo la Changamwe wamekana mashtaka dhidi yao.

Washukiwa Khalif Abdulahi Sigat, James Muli Koti, Joseph Odhiambo Sirawa, Edward Kong Onchonga na Nelson Nkanae, wanakabiliwa na shtaka la kumuua Caleb Ospino Otieno ambaye alifariki dunia katika kituo cha polisi cha Changamwe mwaka wa 2018

Aidha kesi hiyo itasikizwa tarehe 6 na 7 mwezi desimba mwaka huu.

Ikumbukwe kwamba mamlaka ya kutathmini utendakazi wa maafisa wa polisi IPOA ndiyo iliyoidhinisha kushtakiwa kwa watano hao.

BY JOYCE MWENDWA