HabariNewsSiasa

Mwanahabari Mwanaisha Nchipepo Chidzuga kuwania kiti cha ubunge wa Matuga mwaka ujao…..

Familia ya aliyekuwa mwakilishi wa kwanza wa kike kaunti ya Kwale marehemu Zainab Chidzuga imemuidhinisha mwanahabari Mwanaisha Nchipepo Chidzuga kuwania kiti cha ubunge wa Matuga mwaka ujao.

Wakiongozwa na Salim Seif Chidzuga, familia hiyo imesema kuwa imeamua kumuunga mkono Mwanaisha baada ya kukubaliana kwa pamoja.

Kwa upande wake Mwanaisha amewataka wakaazi wa Matuga kumuunga mkono katika azma yake ya kuwania ubunge wa eneo hilo.

Kwa upande wake kakaake mwanahabari huyo Hassan Chidzuga amedai kuwa familia hiyo bado haijakubaliana kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, Hassan amesisitiza kuwa yuko debeni japo ameahidi kumuunga mkono dadaake endapo familia itamchagua.

BY REPORTER