HabariNews

TAKRIBAN ASILIMIA 75 YA WANACHAMA WA BIMA YA NHIF HAWALIPI PESA ZAO KILA MWEZI

Bima ya matibabu nchini NHIF imethibitisha kwamba takriban asilimia 75 ya wakenya waliojisali kuwa wanachama wa bima hiyo hawalipi pesa zao za kila mwezi kama inavyohitajika .

Afisa mkuu wa NHIF Peter Kamunyu amesema hali hii imechangia pakubwa kudorora kwa mapato ya bima hiyo na vile vile kuathiri kwa asimia kubwa utendaji kazi wake akisema sasa wameweka mikakati ya kuwashinikiza wahusika kurejelea malipo yao.

Aidha, Kamunyu amesema kwamba mfumo mpya wa kujisajili kieletroniki kwa walio na NHIF umepunguza visa vya ukora na ufisadi katika bima hiyo uliokuwa unashuhudiwa hapo awali.