HabariNewsSiasa

Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi anapendekeza marekebisho ya sura ya sita ya katiba na sheria ya uchaguzi…

Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi anapendekeza marekebisho ya sura ya sita ya katiba na sheria ya uchaguzi ili kuwafungia nje wawaniaji  wote waliotajwa kwenye sakata za ufisadi.

Wandayi anapendekeza kuwa washukiwa wa ufisadi wasimamishwe kazi hadi pale mahakama itakapoamua kesi zao na iwapo watapatikana kutokuwa na makosa basi wafidiwe kipindi ambacho hawakuwa kazini.

Wakati huohuo Wandayi anapendekeza washukiwa wasiteuliwe kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao.

BY NEWS DESK