HabariMazingiraNews

Jamii zinazoishi gatuzi la Tanariver zimetakiwa kushirikiana kikamilifu katika kutumia maliasili…

Jamii zinazoishi gatuzi la Tanariver zimetakiwa kushirikiana kikamilifu katika kutumia maliasili zinazopatikana maeneo hayo ili kuepuka mizozo ya mara kwa mara.

Mwakilishi wa vijana katika shirika la CICC Yasmini Hassan amesema wakulima na wafugaji wote wana haki sawa kwenye matumizi ya rasilimali kama vile mto Tana kwa shughuli zao za kila siku ikizingatiwa kwamba kiangazi kinazidi kuathiri sehemu mbali mbali nchini.

Vile vile ameelezea umuhimu wa kuheshimiana katika rasilimali kama njia ya kuboresha uhusiano na kudumisha Amani.

Ni kauli iliyoungwa mkono na Ustadh Mohamed Khamis akibainisha wazi kuwa mto ni neema kutoka kwa Maulana na hivyo basi kila mmoja ana haki na uhuru wa kunufaika na neema hiyo.

BY NEWS DESK