AfyaHabariNews

Visa vya ukeketaji vimetajwa kupungua katika kaunti ya Tana River.

Kulingana na naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Tana Delta William Nasongo jamii ambao wanaendelea kutekeleza mila hiyo haramu wanafanyia maeneo ya mashambani kwa usiri.

Aidha Nasongo amesema Visa hivyo vinatekelezwa wakati wa likizo shule zinapofungwa huku akiwaonya jamii dhidi ya kuendeleza ukeketaji wakati shule zikitarajiwa kufungwa kwa likizo wa muhula wa kwanza.

Wakati huo uo Nasongo amesema ipo haja ya kujengwa kwa makao ya kuwanususru wasichana wanaokabiliwa na ukeketaji katika kaunti ya Tana River.

BY NEWS DESK