HabariKimataifaNews

Waasi na wanajeshi 100 wauwawa katika mashambulizi Yemen…

Duru za kijeshi nchini Yemen zinasema karibu waasi 100 nchini humo na wanajeshi wanaoiunga mkono serikali wameuwawa katika kipindi cha saa 48 zilizopita wakati ambapo mapigano yanazidi katika mji muhimu wa Marib.

Kumeshuhudiwa mashambulizi ya angani yaliyofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia yaliyowalenga waasi wa Houthi mjini Marib, hiyo ikiwa ndiyo ngome ya pekee ya serikali iliyosalia kaskazini mwa nchi. Na sasa duru za kijeshi zimeliambia shirika la habari la AFP kuwa Wahouthi 68 na wanajeshi 32 watiifu kwa serikali wamepoteza maisha.

Ni nadra sana kwa waasi hao kutangaza maafa yanayofanyika upande wao ila chombo chao cha habari cha Al-Masirah kimeripoti karibu makombora 60 ya angani katika mji wa Marib siku mbili zilizopita.

BY NEWS DESK