AfyaHabariNews

Serikali ya mombasa kupokea chanjo ya pfizer kutoka marekani hii leo….

Serikali ya kaunti ya Mombasa hii leo inatarajiwa kupokea dozi elfu 35 za chanjo ya covid 19 aina ya Pfizer kutoka serikali ya Marekani.

Shehena ya chanjo hiyo inatarajiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa Moi saa sita adhuhuri.

Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho anatarajiwa kuzipokea chanjo hizo.

Haya yanajiri huku wizara ya afya ikitarajiwa kutoa chanjo ya Pfizer kuanzia wiki ijayo.

BY NEWS DESK