HabariNews

KAFYU YAONGEZWA KWA SIKU 30 ZAIDI.

Marufuku ya kuwa nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri yameongezwa kwa siku 30 zaidi.

Marufuku yaliyokuwa hapo awali yalikamilika tarehe 30 mwezi Septemba pasi na taarifa yoyote kutolewa.

Akizungumza katika kikao na wanahabari kwenye hafla ya kuzindua mtandao wa kupata taarifa kuhusu takwimu za Covid 19 Nchini, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba marufuku haya yameongezwa ili kusaidia Serikali kuanza kuhamasisha watu kuchanjwa kwa wingi kabla ya kuiondoa.

Wakati uo huo Waziri Kagwe amesema masharti yaliyotangazwa na Serikali ya kuzuia msambao na maambukizi ya virusi vya Corona pia yatasalia  yalivyo kwa muda wa siku 30 zijazo.

Haya yakiwa yanajiri huku wito wa marufuku hayo kuondolewa ukizidi kutolewa, Miongoni mwa waliotoa wito huo ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la AMREF Githinji Gitahi ambae amesema kwamba marufuku hayo yamekuwa kikwazo kwa wafanyibiashara usiku na usafiri wa mbali vile vile kuchangia wananchi kuhangaishwa na maafisa na polisi.

BY NEWS DESK