HabariMombasaNews

SERA NA MSIMAMO KWA YALE AMBAYO KIONGOZI AMEYAFANYA KWA WANANCHI NDIO NJIA PEKEE ITAYOMUUZA ASEMA ABULSWAMAD SHARIFF NASSIR.

Akizungumza na wakaazi wa Magogoni eneo bunge la Kisauni Nassir amewataka wakaazi wa Mombasa kuwa macho na kumchagua kiongozi ambaye ana sera na msiamamo kwa yale maendeleo aliyoyafanya kwa wananchi.

Nassir ambaye tayari amekuwa mstari wa mbele kuona kuwa vilio vya wakaazi wa kaunti ya ¬†Mombasa vinasikika,na ambaye yuko kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha ugavana wa jimbo la Mombasa amesema wakaazi wenyewe ndio watakao chagua gavana wao wala hategemei kuidhinishwa[endorse] na kiongozi yoyote kama wengi wanavyodai.

Hata hivyo amesema manifesto yake ni kuona kuwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa na pwani kwa ujumla wameweza kuendelea kiuchumi huku akisisitiza msimamo wake wa kuwa ndani ya chama cha ODM.

Haya yanajiri huku Nassir akiwa na Imani kuwa atarithi kiti cha ugavana wa kaunti ya Mombasa ifikapo mwaka 2022.

BY NEWS DESK