HabariKimataifa

WITO UMETOLEWA KWA VIJANA KOTE NCHINI KUJITOKEZA NA KUSAJILIWA KAMA WAPIGA KURA …

Wito umetolewa kwa vijana kote Nchini kujitokeza na kusajiliwa kama wapiga kura ili kufanikisha idadi inayolengwa kwenye awamu hii ya ujasili ya wapiga kura.

Akizungumza wakati wa kufunguliwa kwa usajili huo Mwenyekiti wa Bajeti ambaye pia ni Mbunge wa Kieni Kanini Kega, amesema kwamba kamati ya bajeti imetoa fedha zitakazowezesha Tume ya Uchaguzi na Mipaka Nchini IEBC kufanikisha zoezi hilo.

Aidha Kanini amekariri kwamba kamati hiyo haitaongeza fedha nyengine kwa ajili ya usajili mwengine wa wapiga kura hivyo kuwaomba Wakenya kujitokeza kwa wingi kusajiliwa wakati huu.

Eneo la Kati linatarajiwa kuwasajili wapiga kura wapya laki sita.

BY NEWS DESK