HabariKimataifaNews

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ABEY AHMED AAPISHWA KUONGOZA MUHULA WA PILI.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameapishwa kuongoza muhula wa pili huku viongozi wachache wa Afrika waliohudhuria hafla hiyo wakimuhimiza kuliweka pamoja Taifa hilo linalokabiliwa na vita vya miezi 11 katika Jimbo la Kaskazini la Tigrey.

Abiy aidha anasema viongozi sita wa Mataifa ya Kiafrika kutoka Nigeria, Senegal, Uganda na Mataifa jirani ya Somalia, Djibout, Kenya na Sudan Kusini wamehudhuria sherehe ya kuapishwa kwake.

Viongozi hao pia wamehimiza amani na kusema Ethiopia inapokosa Amani hata Bara zima la Afrika halitakuwa na Amani

BY NEWS DESK