HabariMichezoNewsSports

WAZIRI WA MICHEZO AMINA MOHAMMED KUFIKA MBELE YA SENETI HII LEO.

Waziri wa michezo Amina Mohammed na wasimamizi wa kamati ya timu ya Kitaifa ya Olympiki NOC wanatarajiwa kufika mbele ya seneti hii leo kufafanua sababu zilizochangia Timu ya Kenya kupata matokeo yasiyoridhisha katika mashindano yasiyoridhisha katika mashindano ya Olympiki ya Tokyo Japan mwaka 2020.

Kamati ya Leba na ustawi wa Umma inayolenga kupata majibu kutoka kwa Waziri Amina kufuatia ombi la Seneta wa Nandi Cherarkey Samson kuhusu maandalizi duni iliyochangia matokeo duni.

Hapo awali seneta Cherarkey alisema baadhi ya wanariadha wa Kenya walihangaishwa na wengine kunyanyaswa hali ambayo ansema iliwasababishia matokeo duni.

Cherarkey anamtaka Waziri Amina na Kamati ya NOCK kueleza ni kwanini Timu ya Kenya ilishindwa kwenye vitengo vya mbio ambazo Kenya imekuwa ikitawala Kimataifa.

BY NEWS DESK