Rais Uhuru Kenyatta ametuzwa na Serikali ya Barbados kwa tuzo ya Order of Freedom of Barbados kutokana na juhudi zake za kuendeleza biashara duniani pamoja na kuimarisha uhusiano kati ya Mataifa ya Bara Afrika na Visiwa vya Caribian.
Tuzo hiyo ya hadhi ya juu ya Taifa hilo hutunukiwa raia wa Babados na wale wa kigeni kwa kutoa huduma za kipekee kwa Taifa la Babados, jamii za Caribian zinazoishi ugenini huku Tuzo hio ikikabidhiwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na Gavana Mkuu wa Taifa hilo Dem Sandra Mason.
Akipokea tuzo hio Rais Uhuru Kenyatta ameeleza kufurahishwa kwake akisema kwamba heshima hio sio yake binafsi bali ishara kuu ya kuonyesha kuimarika kwa uhusiano kati ya Kenya na Barbados.
Wakati uo huo Rais Uhuru ameongeza kwamba Tuzo hiyo inadhihirisha kazi ambayo yeye na Waziri Mkuu Mia Amor Mottley wamekuwa wakitekeleza kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Bara la Afrika, Jamii na visiwa vya Caribian pamoja na Ukanda wa Soko la pamoja la Caricom.
BY NEWS DESK