HabariKimataifaNews

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametangaza baraza lake jipya la mawaziri baada ya kuapishwa siku mbili zilizopita…

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametangaza baraza lake jipya la mawaziri baada ya kuapishwa siku mbili zilizopita kufuatia ushindi wa chama chake kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Juni mwaka huu.

Katika baraza hilo, Abiy amemteua Berhanu Nega – kiongozi wa chama cha ‘Ethiopian Citizens for Social Justice, ambaye ameshinda viti vichache katika uchaguzi huo ameteuliwa kuwa waziri wa elimu.

Belete Molla – kiongozi wa NaMA – naye ameteuliwa kuwa waziri wa masuala ya teknolojia

Hatimaye Kejela Merdasa, – kutoka chama kilichowahi kupigwa marufuku cha Oromo Liberation Front (OLF) – ameteuliwa kushika nafasi ya waziri wa utamaduni na michezo.

Uteuzi mkubwa uliogusa wengi ni ule wa Abraham Belay kutoka chama cha waziri mkuu Abiy cha Prosperity Party (PP) aliyeteuliwa kuwa waziri wa ulinzi huku ikiwa chama cha OLF kikiwa miongoni mwa vyama kadhaa vya upinzani vilivyosusia Uchaguzi huo.

BY NEWS DESK