HabariNewsSiasa

Takriban watu 4486 ndio waliojitokeza kujisajili kama wapiga kura katika Kaunti ya Mombasa hadi kufikia sasa…

Takriban watu 4486 ndio waliojitokeza kujisajili kama wapiga kura katika Kaunti ya Mombasa hadi kufikia sasa. Na haya ni kwa mjibu wa mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir.

Akizungumza  katika kampeni ya kuhamisisha jamii kuhusu umuhimu wa kujiandikisha kama wapiga kura iliyofanyika katika ukumbi wa afisi yake aneo la Majengo hapa Mombasa ,Nassir ameeleza kuwa katika idadi ya kura mpya ambazo zinatarajiwa kuweza kuchukuliwa kaunti ya Mombasa ni laki moja elfu tisini mia mbili thelathini na saba.

Aidha amesikitishwa kuona kuwa tangu zoezi la siku 30 la usajili wa wapiga kura wapya  kuanza ,idadi ambayo imeweza kuchukua kura kaunti ya Mombasa ni ya watu 4486 pekee.

Nassir  ambaye anazidi kuhimiza watu kujisajili kama wapiga kura na ambaye ana gombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa anaamini kushinda kiti hicho kupitia tiketi ya chama cha ODM.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa kaunti ya Mombasa waliohudhuria kampeni hiyo akiwemo mbunge Jomvu Badi Twali,seneta wa kaunti ya Mombasa Mohammed Faki wameshikilia msimamo wao wa kupigia debe mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir kuchukua kiti cha ugavana Mombasa.

Viongozi hao wa ODM aidha wameahidi kukimarisha chama hicho mashinani.

BY NEWS DESK