HabariNewsSiasa

WILIAM RUTO AKUTANA NA VIONGOZI MBALI MBALI KWENYE UKUMBI WA WILD WATERS KAUNTI YA MOMBASA.

Naibu wa Rais Wiliam Ruto amekutana na wagombea wa viti mbali mbali vya uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao katika ukumbi wa Wild Waters Kaunti ya Mombasa kupitia Chama cha UDA hii leo.

Wenyeji hao ambao wanatoka katika Kaunti zote za Pwani wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa faragha na utaanza mda wowote kuanzia sasa.

Miongoni mwa masuala ambayo yanatarajiwa kujadiliwa ni kuhusu namna ya kuendelea kupigia debe chama hicho kwenye eneo la Pwani. Kisha baadae Ruto ataendeleza kampeni zake katika Kaunti ya Kilifi kabla ya kukamilisha ziara yake eneo la Pwani kwenye Kaunti ya Lamu.

Itakumbukwa kwamba ziara ya Ruto katika eneo la Pwani ilianza rasmi siku ya Alhamisi Juma lililopita ambapo alizuru Kaunti ya Taita Taveta, kabla ya kuelekea Kwale, kisha Kilifi na Mombasa.

BY NEWS DESK