HabariNewsSiasa

KINARA WA ODM RAILA ODINGA ATUA MLIMA KENYA KATIKA KAUNTI YA MERU KWA MISURURU YA MIKUTANO.

Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga amemtaka Naibu wa Rais Wiliam Ruto kukomesha madai ya kwamba muafaka wa kisiasa kati yake na Rais Uhuru Kenyatta ndio umehujumu utendakazi wa Serikali ya Jubilee.

Katika mahojiano kwenye kituo kimoja kinachotangaza kwa lugha ya kimeru, Raila badala yake amesisitiza kwamba hayuko kwenye Serikali ya sasa na kwamba hana ushawishi wowote wa kusababisha kukwama kwa shughuli za Serikali.

Wakati uo huo Raila ameirai Serikali kufanikisha azimio la Wakulima wa Miraa huko Meru katika soko la zao hilo ili lifunguliwe tena Nchini Somalia.

Kinara wa Chama Cha ODM Raila Odinga tayari ametua katika Kaunti ya Meru kwa misururu ya mikutano katika eneo hilo na kama ilivyo ada ameanza kwa mahojiano katika vituo vinavyopeperusha matangazo kwa lugha za eneo hilo la Mlima Kenya Mashariki.

Raila ameregela utawala wake wakiwa pamoja na Mwai Kibaki kuwa ishara ya uwezo wake, kuleta mageuzi humu Nchini akitaja suala la madeni katika utawala huo hayakuwa mengi na vile vile waliweza kutekeleza hadi elimu ya msingi bila malipo.

Raila ametumia historia hiyo kutetea mpango wake wa kuwagawia familia maskini ruzuku ya shilingi elfu sita kila mwezi.

BY NEWS DESK