HabariNewsSiasa

Ombi la pili la kumtaka jaji Sankale Ole Kantai kutimuliwa afisini limewasilisha katika idara ya mahakama JSC…

Ombi la pili la kumtaka jaji Sankale Ole Kantai kutimuliwa afisini limewasilisha katika idara ya mahakama JSC na Gabriel Hannah Van Straten ambaye ni dadake marehemu Tob Cohen.

Katika ombi lake Straten ameeleza kwamba jaji Sankale alijihusisha na utovu wa nidhamu kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mkewe marehemu Sarah Wairimu Cohen.

Aidha ameongeza kwamba jaji Sankale alihusika katika kuharibu ushahidi unaowahusha na mauaji ya Tob Cohen kati ya tarehe 20 mwezi Julai na Agosti 28 kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp, mawasiliano ya simu na mikutano ya kupangwa.

Kupitia kwa wakili wake Danstan Omari, Straten anadai kuwa jaji Sankale alimsaidia Sarah Wairimu kuandika na kurekebisha taarifa aliyoandika kuhusiana na kutoweka kwa kakake Tob Cohen.

Haya yanajiri baada ya mwanaharakati Okiya Omtata kuwasilisha ombi sawia na hili la kutaka kuondolewa afisini kwa jaji Sankale.

BY NEWS DESK