HabariKimataifaNews

Rais wa Malawi Lazarus Chikwera amewasili nchini kufuatia ziara yake rasmi ya siku tatu.

Rais wa Malawi Lazarus Chikwera amewasili nchini kufuatia ziara yake rasmi ya siku tatu.

Rais Chikwera ameandamana na mkewe Monica Chikwera huku akitazamiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mashujaa hapo kesho katika uwanja wa Wang’uru katika kaunti ya Kirinyaga.

Walipowasili, wamepokewa na Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa na mwenzake wa ICT Joe Mucheru.

Rais Uhuru Kenyatta na mama wa taifa Margret Kenyatta wanatarajiwa kumpokea na kumkaribisha rasmi rais Chikwera na mkewe siku ya alhamisi katika ikulu ya rais.

Aidha watu 2000 pekee ndio watakaoruhusiwa kuhudhuria Sherehe hizo za mashujaa ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona.

Uwanja wa Wang’uru utafunguliwa saa kumi alfajiri.

BY NEWS DESK