HabariKimataifaNews

Mamia ya wanafunzi wamelivamia bunge nchini DRC wakitaka walimu wao waongezewe mishahara.

Mamia ya wanafunzi wamelivamia bunge nchini DRC wakitaka walimu wao waongezewe mishahara.

Wanafunzi hao walikuwa wanapeperusha matawi na pamoja na mabango yaliyoandikwa tunataka kusoma na ikiwa hatutasoma, tutatumia dawa za kulevya.

Walimu wamekuwa mgomoni tangu Oktoba 4, mwanzoni mwa masomo mwaka huu wakitaka waongezewe mshahara na kupunguza umri wa kustaafu pamoja na masuala mengine.

Serikali imewashutumu viongozi wa dini ambao wanasimamia shule nyingi za msingi , kwa kudai kuwa wanahusika na mgomo huo ingawa viongozi hao wamekanusha madai dhidi yao.

Makamu wa rais wa Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo Jean-Marc Kabunda, amewataka wanafunzi kurudi nyumbani maana haya sio mapambano yao.

BY NEWS DESK