HabariNewsSiasa

Mbunge wa mvita Abdulswamad Shariff Nassir ametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Mombasa kuondoa ushuru unaotozwa kwa bidhaa za chakula.

Mbunge wa mvita Abdulswamad Shariff Nassir ametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Mombasa kupitia gavana Hassan Ali Joho kuondoa ushuru unaotozwa kwa bidhaa ya Tomato na Viazi miongoni mwa bidhaa nyengine za chakula katika Kaunti hiyo.

Akizungumza kwenye kampeni ya kuhamasisha wakaazi wa Mombasa kuendelea kujisajili kama wapiga kura, Nassir amesema kwamba tayari Gavana Joho ashakubaliana na wito huo kwani hali ya mapato kwa wakaazi wa jimbo la Mombasa na pwani kwa ujumla yamezorota,huku wakaazi wengi wakiumia kufuatia kupanda kwa gharama za kiuchumi..

Nassir aidha ameeleza kuwepo kwa hali ya afueni kwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa endapo serikali hiyo itatilia maanani wito huo na kupunguza ushuru kwa bidhaa za chakula kaunti ya Mombasa.

Haya yanajiri baada ya gavana Hassan Ali Joho kuondoa ushuru kwa bidhaa ya Miraa inayoingia mjini Mombasa.

BY NEWS DESK