HabariNews

SHUGHULI ZA MASOMO KATIKA SHULE YA UPILI YA MWAMGUNGA ENEO LA GOLINI ZASITITISHWA…

Shughuli za masomo katika shule ya upili ya Mwamgunga eneo la Golini kaunti ya Kwale zimesititishwa baada ya wanafunzi kugoma.

Wanafunzi hao wanaolalamikia nyongeza ya karo na chakula kisichofaa pamoja na ukosefu wa maji eneo hilo huku wakiandama pamoja na wazazi wakitatiza shughuli za uchukuzi katika barabara kuu ya Kombani kuelekea mjini Kwale.

kulingana na wazazi hao  shule hiyo imeongeza karo bila ya wao kushirikishwa na kuongeza kuwa wanafunzi hawapati chakula pamoja na maji.

Aidha mwalimu mkuu wa shule hiyo Winrose  Mwanike  amepuzilia mbali madai ya wazazi hao akisema kwamba wazazi hao hawataki kulipa karo kwa wakati unaofaa.

BY NEWS DESK…