HabariNews

IDARA YA USALAMA KUCHUNGUZA KISA AMBAPO MWANAFUNZI WA DARASA LA ANNE ARIPOTIWA KUJINYONGA HUKO MALINDI .

Idara ya usalama mjini malindi imetakiwa kuchunguza kwa kina kisa ambapo mwanafunzi wa darasa la nne anadaiwa kuaga dunia kwa kujinyonga katika kijiji cha Mtangani viungani huko wiki moja iliyopita.

Kulingana na babake marehemu Samuel Safari mwanawe alikuwa buheri wa afya kabla kupatikana ameaga dunia.

Safari ameitaka idara ya upelelezi wa jinai kuingilia kati na kuchunguza kisa hicho akimtaja mwanawe kama tegemeo katika familia hiyo.

Hadi kifo chake, mwendazake kwa jina Moses Charo alikuwa mwanafunzi katika shule ya msingi ya Majivu akiwa darasa la nne.

Aidha kulingana na majirani mwanafunzi huyo alionekana akicheza na wenzake barabarani mda mfupi kabla mwili wake kupatikana ameaga dunia.

Wamedai huenda marehemu alikuwa akicheza na kamba huku wenzake wakidaiwa kutoroka baada ya kisa hicho.

Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi eneo hilo John Kemboi amesema maafisa wake tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.

BY NEWS DESK