HabariMombasaNewsSiasa

GAVANA WA MOMBASA ALI HASSAN JOHO AWAHAKIKISHIA WAKAAZI WA MOMBASA HATI MILIKI.

Gavana wa mombasa ali hasaan joho amewahakikishia wakazi wa kaunti ya mombasa kuishi na amani bila kufurushwa kama maskuota akisema kuwa serikali yake imjipanga  vilivyo katika kuhakikisha kila mmiliki wa ardhi anapata hati miliki.

Amesema  hayo aliko kuwa katika uwanja mwahima kaunti ndogo ya likoni kwenye shughuli ya kuwapa wenyeji hao hati miliki.

Huku zoezi hilo hii leo likielekezwa katika kaunti ya ndogo ya jomvu ambako wenyeji wa eneo wanaohishi ekari zaidi ya mia moja watapata fursa ya kupata hati miliki hizo.

Ikumbukwe kwamba swala la hati miliki katika kaunti za Pwani limekuwa ni gumzo kila kukicha wenyeji wakifurushwa kila uchao kutokana na ukosefu wa cheti hizo.

Wakaazi wa eneo hilo aidha ni  kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi kwa hofu ya kufurushwa na maskwota waliokuwa wakidai kumiliki ardhi hio yenye takribani hekari 294.7.

Akizungumza kwenye hafla ya kuwapokeza hatimiliki wakaazi wa eneo la Kinduguni ,hafla iliyofanyika katika uwanja wa Mwahima eneo bunge la Likoni,Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Ali Joho amehakikishia wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuwa hakuna atakaye furushwa kwenye makaazi yao wakati akiwa kwenye hatamu ya uongozi.

Ameyasema haya kutokana na kuwa baadhi ya wakaazi wameishi kwenye mashamba yao kwa takribani miaka 20.

BY NEWS DESK