HabariLifestyleNews

WAAZAZI WAOMBWA KUSHIRIKIANA ILI KUPUNGUZA MIMBAZA MAPEMA.

Wazazi katika eneo bunge la Kaloleni wametakiwa kushirikiana na walimu ili kukabiliana na ongezeko la mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi .

Kwenye hotuba yake wakati wa kupeana basi  lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 67 kwa shule ya upili ya Moi Kadzonzo,mbunge wa eneo hilo Paul Katana amesema jukumu la kuchunga wanafunzi sio la walimu pekee.

Kauli ya Katana inajiri wakati ambapo idadi ya mimba za mapema katika sehemu hiyo imeripotiwa kuongezeka maradufu.

BY NEWS DESK.