HabariNewsSiasa

GAVANA WA KAUNTI YA KIRINYAGA ANNE WAIGURU AJIUNGA NA CHAMA CHA UDA.

Gavana wa Kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru amejiunga na chama cha UDA baada ya kukutana na Naibu Rais William Ruto katika makaazi yake mtaani Karen, Jijini Nairobi.

Waiguru ambaye ananuia kupigania tena nafasi ya ugavana katika Kaunti hiyo, ameandamana na wawakilishi wadi 23 na ambaye kwa sasa ni rasmi kwamba ni mwanachama wa UDA.

Itakumbukwa kwamba siku chache zilizopita gavana huyo alikuwa amedokeza kwamba angeachana na kambi ya Rais Uhuru Kenyatta na kujiunga rasmi na mrengo wa naibu rais maarufu kama “Hustler nation”.

BY NEWS DESK