HabariNews

Shule ya upili ya wavulana ya Dr. Kraph ilioko Rabai katika kaunti ya Kilifi imefungwa kwa mda usiojulikana

Shule ya upili ya wavulana ya Dr. Kraph ilioko Rabai katika kaunti ya Kilifi imefungwa kwa mda usiojulikana kufuatia kuteketea kwa bweni moja shuleni humo.

Inaarifiwa kwamba, moto huo ulizuka usiku wa kuamkia leo huku baadhi ya wanafunzi kupata majeraha madogo walipokuwa wakikimbilia usalama wao.

Haya yanajiri huku Shule ya upili ya Golini katika kaunti ya Kwale ikikadiria hasara baada ya moto kuteketeza bweni moja usiku wa kuamkia leo.

Hakuna mwanafunzi aliyejeruiwa kwenye mkasa huo huku uchunguzi ukianzishwa kubaini chanzo cha moto huo.

BY NEWS DESK