Takriban vijana 3,400 watasajiliwa katika Awamu ya Tatu ya mpango wa Kazi Mtaani ili kusaidia katika mpango wa kudhibiti malaria katika kaunti tofauti kufuatia agizo la Rais Uhuru Kenyatta.
Kulingana na Mshauri Mkuu katika Muungano wa Viongozi wa Afrika kuhusu Malaria Willis Akhwale, vijana hao watatumwa katika kaunti 16 ambazo vinashuhudia visa vingi vya malaria.
Wakati wa sherehe za siku ya Mashujaa wiki jana, Rais Kenyatta aliagiza Hazina ya Kitaifa kutenga Shilingi bilioni 10 kwa mpango huo wa Kazi Mtaani.
Haya yanajiri huku huku idadi ya wakenya wanaotumia vyandarua vya kuzuia mbu nchini ikishuka hadi asilimia 14.
Haya ni kwa mujubu wa mkuu wa idara ya kitaifa ya mpango wa malaria George Githuka.
BY NEWS DESK