HabariNewsSiasa

IEBC yasema haitaongeza muda wa usajili wa umma unaoendelea kote nchini…

Licha ya kwamba idadi ndogo ya wapiga kura wapya wamesajiliwa katika zoezi la usajili umma linaloendelea kote nchini, tume huru ya uchaguzi IEBC imesema kuwa muda hautaongezwa.

Kamishna wa IEBC Francis Wanderi amesema shughuli hiyo itakamilika rasmi tarehe 2 mwezi Novemba kama ilivyoratibiwa.

Kulingana na Wanderi ni kwamba IEBC haina fedha za kutosha kufaulisha shughuli hiyo iwapo muda huo utaongezwa.

Akizungumza katika kaunti ya Kericho, Wanderi sasa amewashauri wakenya wenye umri wa miaka 18 na zaidi kujitokeza kwa wingi ili kusajiliwa kuwa wapiga kura.

By Joyce Mwendwa