HabariSiasa

Wakaazi wa Makumba Magarini kaunti ya Kilifi wameitaka serikali kubuni mbinu mbadala za kukabili ukame…

Wakaazi wa Makumba Magarini kaunti ya Kilifi wameitaka serikali kubuni mbinu mbadala za kukabili ukame katika eneo hilo kama kuchimba visima ili kuendeleza shughuli za kilimo katika eneo hilo.

Kulingana nao juhudi za serikali kuwafadhili kwa chakula hazijafua dafu kwani chakula hicho hakitoshi kwa wakaazi hao.

Mwaniaji wa kiti cha useneta kaunti ya kilifi George Kithi ametoa wito kwa wakaazi wa kilifi, serikali kuu na hata dunia nzima kwa ujumla kujitokeza na kuwapa msaada ili kuwafaidi watu wote ukanda wa pwani.

Aidha ameahidi kuwa hatua mbadala zitachukuliwa kuhakikisha kuwa wakaazi wanaoathirika wanafaidika.

BY NEWS DESK