HabariNews

WAKILI TAJIKA HASSAN NANDWA APATIKANA.

Wakili Hassan Nandwa ambaye aliripotiwa na familia yake kutoweka tangu tarehe 28 Mwezi Oktoba Mwaka huu amepatikana.

Kwa mujibu wa viongozi wa Msikiti wa Jamiya Jijini Nairobi ni kwamba Nandwa amepatikana Mjini Mwingi baada ya kuachiliwa huru na waliokuwa wamemteka nyara.

Wakati uo huo aliyekuwa mteja wake Elgiva Bwire ambaye vile vile aliripotiwa kutoweka, hajajulikana alipo kufikia sasa.

BY NEWS DESK