HabariNewsSiasa

VYAMA VYA ODM NA JUBILEE KUWASAILISHA WAGOMBEAJI KAUNTI YA NAIROBI.

Vyama vya ODM na Jubilee vinatarajiwa kuamua jinsi ya kuwawasilisha wagombeaji katika Kaunti ya Nairobi na viti vyengine kote Nchini kufuatia ushirikiano unaotarajiwa kuafikiwa.

Akizungumza kabla ya kuhudhuria ibada katika Kanisa la Lejo Maria Makongeni, Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga amesema kwamba mpango wa kuwa na asilimia kubwa ya wawakilishi wadi ya Nairobi, miongoni mwa mikakati inayowekwa ili kuhakikisha Vyama hivyo vina ushawishi Nairobi na kote Nchini kwa ujumla.

Wakati uo huo Odinga amesema kwamba atatangaza mustakabali wake wa kuwania urais kwenye uchaguzi Mkuu ujao ifikapo tarehe tisa mwezi ujao wa Disemba.

Akizungumza wakati wa Kampeni zake jijini Nairobi Raila amesema kwamba atawapa fursa wakenya kumchagulia naibu wake kwenye kinyangányiro cha urais.

Odinga aidha , amewahakikishia wakenya kwamba iwapo atachaguliwa kuwa Rais, basi atakamilisha ahadi yake ya kuwapa familia zisizojiweza  ruzuku shilingi 6,000 akipuzilia mbali mpango wa bottom up unaoungwa mkono na naibu wa rais.

BY NEWS DESK