HabariKimataifaNews

Seif al- Islam al-Gaddafi atangaza rasmi azma ya kugombea urais wa Libya…

Mtoto wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba wenye lengo la kumaliza miaka kadhaa ya machafuko tangu baba yake alipoondolewa madarakani.

Seif Al- Islam Al-Gaddafi mwenye umri wa miaka 49, amejitokeza na kuonekana katika mkanda wa vidio uliotolewa na ofisi inayosimamia uchaguzi, akitia saini nyaraka katika kituo cha uchaguzi kusini mwa mji wa Sebha.

Baadhi ya wagombea wengine ni pamoja na kamanda wa kijeshi upande wa mashariki Khalifa Haftar, waziri Mkuu Abdulhamid al-Dbeibah na spika wa bunge Aguila Saleh.

Jina lake ni miongoni mwa majina yanayojulikana sana Libya, na amekuwa na jukumu kubwa katika sera za nchi hiyo kabla ya vuguvugu la mwaka 2011 lililoungwa mkono na Jumuiya ya kujihami NATO na kuharibu utawala wa familia yake.

Seif amekuwa nje ya macho ya umma kwa karibu muongo mmoja.

BY NEWS DESK