HabariNews

Wahudumu wa bodaboda kaunti ya Kwale wametakiwa kutumia vipaji vyao kujiendeleza kimaisha…

Wahudumu wa bodaboda kaunti ya Kwale wametakiwa kutumia vipaji vyao kujiendeleza kimaisha badala ya kujihusisha na utumizi wa dawa za kulevya.

Mwenyekiti wa wahudumu hao kaunti ya Kwale Nehemiah Kinywa amewataka waendeshaji wa bodaboda kutumia vipaji vyao kama njia mbadala ya kujikimu kimaisha.

Kinywa amewataka vijana wa bodaboda kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika mashindano ya kutambua vipaji ya Kwale Got Talent yanayoendelea kaunti hiyo.

Kwa upande wake afisa mkuu mtendaji wa mashindano hayo Vincent Okeyo amesema kuwa vijana watatumia vipaji vyao kujitegemea kimaisha.

Okeyo amesema kwamba wanalenga kuwaelimisha vijana kuhusu athari ya utumizi wa dawa za kulevya na mimba za mapema.

BY NEWS DESK