HabariNews

Milipuko miwili yatokea katikati mwa jiji la Kampala nchini Uganda.

Katika taifa jirani la Uganda milipuko miwili imetokea nchini humo.

Inaarifiwa kwamba mlipuko mmoja umetokea kwenye jumba la maduka karibu na kituo cha Polisi cha Central na mwingine karibu na Bunge la taifa hilo.

Watu kadhaa wanaripotiwa kufariki huku wengine wakijeruhiwa na hali ya taharuki ikitijwa kutanda.

Vikosi vya usalama vimezingira eneo la tukio na kuanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha milipuko huo na vilevile iwapo ni shambulizi la Kigaidi.

Ikumbukwe mwezi uliopita, palitokea milipuko miwili tofauti nchini humo na ambayo iliwaua watu wawili mmoja alikuwa ni mhudumu katika baa na mwingine, mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alikuwa ameingiza vilipuzi kwenye basi.

BY NEWS DESK