Kulingana na upande wa mashtaka wamesema kwamba Mwendwa aliondolewa katika Wadhifa huo majuma matatu yaliyopita na hivyo basi hana kesi ya kujibu baada ya uchunguzi wa kesi hiyo kukamilika huku Hakimu mkuu Wandia Mwendwa akiagiza kufungwa kwa kesi hiyo.
Kupitia uamuzi ambao umetolewa hii leo, mahakama imeagiza kwamba Mwendwa aregeshewe kiasi cha pesa cha shilingi milioni 4 alizolipa kama dhamana alipoachiliwa.
Mawakili wake wakiongozwa na Erick Mutua, Nelson Havi, Tom Ojienda na John Haminwa, hawakupinga hatua ya upande huo wa mashtaka kumuondolewa kesi mteja wao.
Itakumbukwa kwamba mahakama ilikuwa imewapa upande wa mashtaka muda wa siku 7 kuwasilisha mshataka dhidi ya mwendwa au kesi itupiliwe mbali huku Waziri wa michezo Amina Mohammad aliivunja bodi ya FKF na kubuni kamati ya muda ya kusimamia shughuli za shirikisho hilo.
Mwendewa alikuwa anakabiliwa n atuhuma za ufisadi na utumizi mbaya wa ofisi yake.
BY NEWS DESK