Baraza la wazee kutoka kata ndogo ya Mji wa kale kaunti ya mombasa wanalalamikia mabomba ya maji taka wanaodai kuwa yameharibika na kuchafua mazingira katika mji huo na hakuna anayeshughulikia kuyarekibisha.
Akizungmza na meza yetu ya habari baraza hilo kupitia Mzee Shebe ambae ni mmoja wa wakazi katika sehemu hiyo anasema kuwa jamii zinazoishi katika mji huo zimetengwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na kugeuka kuangalia maslahi yao na kuwasahau wananchi.
Wakati huo Abdallah Razini anadai kuwa imefikia wakati hata na serikali za kaunti kuwatenga kutokana na kutohudumiwa kikamilifu kama inavyoshuhudiwa katika sehemu zingine
BY DAVID OTIENO