Walemavu katika kaunti ya Kwale wamelalamikia kutengwa na serikali ya kaunti ya Kwale katika maswala ya ajira kufuatia ukosefu wa uwakilishi katika serikali.
Wakiongozwa na Sofia Wedo, wamedai kuwa serikali ya kaunti hiyo haijazingatia sheria ya asilimia 5 ya uajiri kwa watu wanaoishi na uwezo maalum.
Walemavu hao wamedokeza kwamba hali hiyo imechangiwa na hatua ya serikali ya kuwatenga katika maswala ya uongozi.
Kwa upande wake afisa wa baraza la watu wanaoishi na ulemavu katika kaunti ya Kwale Koima Chimera amesema kuwa kwa sasa wanashinikiza utekelezaji wa sheria hiyo.
Chimera amedokeza kwamba tayari baraza hilo linashirikiana na mashirika ya kijamii ili kutetea haki za walemavu katika kaunti hiyo.
BY NEWSDESK