HabariMombasaNews

MATUMAINI YA KUOKOLEWA KWA MWILI WA MTOTO ALIYETUMBUKIA NDANI YA KISIMA INAENDELEA KUFIFIA.

Matumaini ya kuopolewa kwa mwili wa Fadhili Rama mtoto aliyetumbukia ndani ya kisima eneo la Bakarani Kaunti ya Mombasa siku tano zilizopita inaendelea kufifia.
Shimo hilo lilikuwa limefunikwa kutumia vipande vya zulia vya plastiki yaani plastic carpet.
Benard Opondo amesema kwamba familia yake ambao ni rafiki kwa familia ya Rama inatoka eneo la Mtwapa katika Kaunti ya Kilifi ilikuwa imeiialika kwa sherehe za krisimasi huku akivishinikiza vitengo vinavyohusika kuwasaidia kuuopoa mwili wa Fadhili Rama
Itakumbukwa kwamba Rama, mtoto mwenye umri wa maika miwili alitumbukia siku ya tarehe 25 majira ya saa kumi jioni alipokuwa akicheza na watoto wenzake.

BY NEWSDESK