HabariNewsTravel

WATAKAO SAFIRI KUTUMIA BARABARA YA LAMU GARSEN KWA SHEREHE ZA MWAKA MPYA WATALAZIMIKA KUBEBA STAKABADHI ZA URAIA.

Watakao safiri kutumia barabara ya Lamu Garsen kwa sherehe za mwaka mpya watalazimika kubeba stakabadhi za uraia ambazo wataziwasilisha kwa vitengo mbalimbali vya usalama vinavyo simamia maeneo mbalimbali ya barabara hiyo.
Kulingana na kamishina wa Lamu Irungu Masharia wanaosafiri shariti wabebe vitambulisho vyao vya kitaifa au passpoti kudhibitisha kwamba ni watalii.
Hata hivyo wazazi watalazimika kubeba vyeti halisi vya kuzaliwa vya watoto wanaosafiri nao kwa wale ambao hawajapata vitambulisho vyao,na wale ambao wamefikisha umri wa miaka kumi 18 na zaidi watalazimika kubeba kadi za kusubiri kupata vitambulisho vyao kutoka ofisi husika za serikali.
Aidha stakabadhi hizo zitawasilishwa kwa maafisa wa vitengo vya usalama wanaoshika doria katika vizuizi vya barabarani,ambavyo vimewekwa ili kuimarisha usalama kaunti hiyo.
Ilivyo sasa kuna vituo vya ukaguzi wa magari na watu na usafari kutumia barabara hiyo ambavyo viko kwenye maeneo ya Ndewu, Itsowe, Gamba na Wito.

BY NEWSDESK