HabariKimataifaNews

MAELFU WAANDAMANA NCHINI UJERUMANI KUPINGA VIZUIZI VIPYA VYA KUPAMBANA NA COVID-19.

Maelfu ya watu wameandamana kwenye mitaa ya miji mbalimbali nchini Ujerumani kupinga vizuizi vipya na vikali vilivyotangazwa na serikali kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.
Wakaazi wa upande wa mashariki ya Ujerumani ndiyo walijitokeza kwa wingi kuhudhuria maandamano hayo ambapo polisi imesema katika jimbo la Mecklenburg-Vorpommern pekee, zaidi ya waandamanaji 15,000 waliteremka mitaani.
Maandamano ya maelfu ya watu yamefanyika pia katika miji kadhaa ya majimbo ya Brandenburg, Saxony-Anhalt, Lower Saxony, Hesse, Rhineland-Palatinate na hata Thuringia.
Haya yanajiri baada ya serikali ya nchi hiyo kutangaza vizuizi vikali zaidi vitakavyoanza kutekelezwa hii leo hususan katika majimbo 8 miongoni mwa 16 nchini Ujerumani, taifa ambalo sasa linapambana na wimbi la tano la maambukizi ya kutisha ya covid-19

BY NEWSDESK