AfyaHabariNews

Miungano mbalimbali ya madaktari nchini imekutana kujadili hatua ya bima ya kitaifa ya afya ya NHIF.

Miungano mbalimbali ya madaktari nchini imekutana kujadili hatua ya bima ya kitaifa ya afya ya NHIF kutoa kandarasi mpya kwa wahudumu wa afya na kupunguzwa kwa matibabu ya wenye matatizo ya figo yaani dialysis.
Wakiongozwa na katibu mkuu wa chama cha madaktari KMPDU W. Otela na Okem Were,wahudumu wamesema kwamba matakwa ya kandarasi hiyo sharti yatekelezwe,kwani uamuzi huo hawakuwahusisha washikadau wote katika sekta ya afya.
Hata hivyo madaktari hao wamesema kwamba kandarasi hiyo imekataliwa na hospitali binafsi na hata hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi,kwani haijasimamia magonjwa yote na watakao taabika ni wakenya wanaotegemea NHIF.
Aslimia 90 ya hospitali nchini hazijakubaliana na mkataba utakao dumu hadi mwaka 2024, vile vile NHIF imeagiza hospitali hizo kutia saini ifikiapo tarehe 31 ya mwezi huu.
Aidha hospitali hizo zisipotia saini basi kuazia januari mosi wakenya hawatapata huduma kupitia cadi ya NHIF.

BY NEWSDESK