HabariNewsSiasa

Spika wa bunge la kaunti ya kwale Sammy Ruwa atangaza azma yake ya kuwania ugavana.

Spika wa bunge la kaunti ya kwale Sammy Ruwa, ni wa hivi punde kutangaza azma ya kutaka kumrithi gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya mwaka 2022.
Akizungumza katika eneo la Matuga, Ruwa amesema yuko katika kinyang’anyiro hicho na kuahidi kutatua suala tata la umiliki wa ardhi katika kaunti hiyo, huku akiahidi kurudisha ardhi zote zilizonyakuliwa na mabwenyenye.
Wakati uo huo spika huyo amesema kwamba analenga kuwekeza zaidi katika kunawirisha viwanda katika kaunti hiyo ili kupunguza msongamano wa ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana.

BY NEWSDESK